ushuda wa kweli
ushuda wa kweli
usikate tamaa
Niliingia kwenye Ukristo nilipofikisha miaka 18. Nilizaliwa kusini
mwa Urusi. Nilimpenda sana Yesu, na nikawa na bidii sana
Kanisani, nikabatizwa kwa Roho Mtakatifu na nikawa nawashuhudia
watu Injili. Mungu amenibariki sana.
Mungu aliponibatiza kwa Roho Mtakatifu nilipata shauku kubwa
sana ya kuwashuhudia watu habari za Yesu. Nilikuwa nikiongea
Habari Njema za Yesu karibu kila siku. Nilijihisi niko karibu sana na
Mungu. Nilitumia saa nyingi kuomba na kusoma Biblia.
Wakati fulani nilipatwa na jinamizi. Niliota kuwa ibilisi ananifukuza.
Aliapa kuwa ni lazima atanipata. Nilipozinduka usiku ule, hofu
haikuondoka. Badala yake ilizidi kuongezeka. Hofu iliongezeka sana
kiasi kwamba nikawa nimechanganyikiwa kabisa. Nilijua kuwa niko
katikati ya uovu. Nilikuwa chumbani kwangu, lakini ilionekana kana
kwamba niko mahali pengine kabisa. Nilianza kuhangaika kuomba
na kumsifu Mungu. Hili lilikuwa ni jambo pekee lililonifanya nibakie
na akili zangu timamu. Niliomba karibia usiku kucha. Ile hali ya
uovu ilikuja kuondoka asubuhi.
Nilipomsimulia jambo lile mmoja wa wamisionari wa Kimarekani
kanisani kwangu, aliniambia kuwa ibilisi amefungwa na kuwa
hana uwezo wa kumdhuru Mkristo yeyote. Nilikuwa sijawahi
kufundishwa chochote kuhusiana na vita vya kiroho na sikujua
kuwa nilitakiwa kufanya kitu ili kumpinga adui. Nimekuja kujifunza
ukweli huo kwa njia ngumu kabisa. Ni miaka mitatu baadaye ndipo
nilipofahamu kuwa ibilisi yu hai na yuko duniani; na anachukia sana
na kushindana na kila mmoja anayeamua kuyatoa maisha yake kwa
Yesu Kristo.
Muda mfupi baada ya kupata ubatizo wa Roho Mtakatifu, kwa ndani
moyoni, nilianza kujiona kuwa mimi nilikuwa mtu maalum sana
kwa Mungu kuliko Mkristo mwingine yeyote au watu wengine.
Nilianza kuhisi hivyo kwa sababu ya baraka zote za kimwili na
kiroho alizonipa Mungu. Kazi yangu ya ukufunzi ilikuwa inakua
kule Urusi; nilipokea fedha kwa ajili ya kusafiri ng’ambo, na zaidi
ya hapo, nilipewa skolashipu kamili ya kwenda kusoma Chuo Kikuu
cha Columbia kule New York.
Siku moja wakati nikiomba, Mungu aliniambia kuwa ninatakiwa
kutubu. Mungu alinionya kuhusiana na majivuno yangu na
kuniambia nitubu, vinginevyo NINGEANGUKA. Alisema kuwa mimi
sikuwa mtu maalum kuliko mtu mwingine yeyote. Pia aliniambia
niache kuwahukumu wengine. Kwa bahati mbaya, mimi nilikuwa
nimesisimka zaidi kutokana na ukweli kwamba Mungu anasema
nami badala ya ukweli kwamba nilitakiwa kumtii na kufanya kile
anachoniambia.
Kuishi katika jiji la New York...
Miaka minne iliyopita, toka tarehe ya kuandikwa kwa ushuhuda
huu, nilienda New York ili kusomea shahada ya pili kwenye Chuo
Kikuu cha Columbia. Nikiwa New York, mambo hayakwenda kama
nilivyokuwa nimetarajia. Nilikuwa na vita vikubwa na sikuelewa
kwa nini Mungu aliruhusu nipitie mateso kiasi hicho. Japokuwa
Mungu alinibariki sana kwa skolashipu kamili kwenda kusomea
Columbia, sikumwamini na wala sikumshukuru wakati wa mapito
yangu magumu. Badala yake, nilipachukia New York na Columbia
na nikaanza kunung’unika na kulalamika sana.
Huu ulikuwa ndio mwanzo wa kuanguka kwangu. Niliingiwa na
huzuni kubwa sana na nikawa katika maumivu na hofu kubwa.
Nilifunga, nikaomba mara kwa mara, nikasoma Biblia, nikaenda
kanisani, lakini maumivu na hofu ile havikuondoka! Hali ile
ilikuwa inatia uchungu moyo wangu kiasi kwamba ikawa ni vigumu
kwangu kutembea au kuzungumza. Kila dakika ilihitaji nguvu
sana. Ilikuwa ni kama vile mtu ananivuta chini na kunizuia kupiga
hatua. Muda wote nilikuwa nanyanyaswa na ibilisi ambaye alikuwa
akiniambia kuwa mimi nimeshashindwa kabisa.
Baada ya mwaka mzima wa mateso yangu, Mungu alinivuta tena
kwake kwa muda mfupi. Alizungumza nami na nikaandika maneno
yake kwenye kitabu changu cha kumbukumbu. Ni kwa miaka miwili
tu ndio nilielewa kile alichokuwa ameniambia. Mungu aliniambia
kuwa nitapitia majaribu makali sana na kwamba ningeteseka sana,
lakini aliahidi kunivusha katika yote hayo na kuleta mabadiliko
yenye matunda mema ndani yangu.
Wakati nilipokuwa naisikia sauti ya Mungu, nilikuwa naweza pia
kusikia sauti za mapepo. Nilikuwa sijui kabisa kwamba mapepo
yanaweza kuiga sauti ya Mungu ili kuwadanganya Wakristo.
Sikujua kuwa natakiwa kulijaribu kila neno kwa njia ya Biblia.
Ndiyo maana, niliposikia kuwa ningeenda kufanya mafunzo ya
vitendo kwenye Benki ya Dunia na kwamba ningekutana na
mume wangu wa baadaye kule D.C, niliamini kuwa hayo yanatoka
kwa Mungu. Kumbe pepo alikuwa anasema na tamaa zangu za
kimwili. Niliyapenda maneno hayo na nikayaamini. Nilikuwa na
mashaka, lakini pia nilidhani kwamba Mungu hawezi kuruhusu pepo
anidanganye.
Muda mfupi baada ya hapo, rafiki yangu pekee Mkristo wa New
York aliondoka kwenda kwenye mapumziko ya majira ya joto.
Nilibakia peke yangu. Japokuwa nilikuwa nimeshakaa kwenye
jiji hilo kwa mwaka mzima, bado sikuwa na marafiki wa Kikristo.
Nilihudhuria kanisani, lakini sikuwa namfahamu yeyote pale.
Nilijawa na huzuni zaidi. Nilikuwa peke yangu kabisa na sikuwa na
mtu wa kumshirikisha mashindano yangu. Nilidhani kuwa Mungu
alikuwa hajali na hakunipenda tena kwa kuwa hakujibu maombi
yangu ya kupata kanisa na kuwa na marafiki wa Kikristo. Niliishiwa
na nguvu kabisa pale niliposhindwa kwenye usaili kwenye Benki
ya Dunia na kukosa kazi. Sikuelewa kwa nini Mungu aliruhusu
pepo anidanganye. Sikuwa na hamu ya kuishi tena na nikaanza
kuwaza juu ya kujiua! Sikuweza kabisa kustahimili maumivu yangu
yasiyokoma.
Kisha nilitambua kuwa nisingeweza kufa kwa sababu nikijiua
ningeenda jehanamu na kutumbukia kwenye mateso makubwa
zaidi, tena ya milele! Nikajiona kama mtu aliyenaswa. Kuishi sitaki
lakini wakati huohuo kujiua nako siwezi. Nilijihisi kama vile niko
jehanamu. Maumivu yalikuwa makali sana kiasi kwamba nilianza
kujikata kwa kisu, maana maumivu ya kimwili yalionekana kwangu
kuwa ni mepesi kuliko mateso ya moyoni mwangu. Uovu ulikuwa
wakati wote umenizunguka, ukipenya ubongo wangu, ukinitesa
moyo wangu, wakati wote ukiwa tayari kusema nami na kuniburuta
chini! Kadiri nilivyozidi kuomba na kusoma Biblia, ndivyo nilivyozidi
kuteswa na hizo sauti, na ndivyo maumivu yalivyozidi. Sikujua cha
kufanya na sikuwa na jinsi ya kuzuia!
Ndipo nilifanya jambo ambalo si la kawaida. Sikuwa na uwezo wa
kustahimili maumivu zaidi ya hapo, hivyo nikawa nimeanguka
kabisa. Nilijawa na hasira sana dhidi ya Mungu kiasi kwamba
nikamwambia aondoke kwangu na aachane nami! Nilimwambia
kuwa simpendi na sikuwa tayari kuzungumza naye tena wala kuwa
naye. Kwa kuwa nilikuwa ni mtu wa kuzungumza naye kila wakati,
ilibidi nijilazimishe sana kuacha kumfikiria. Niliacha kuomba na
kusoma Biblia. Nikaamua kufuata njia zangu mwenyewe. Sikuwa
najua sawasawa madhara ya hatua yangu hiyo. Sikujua kuwa
nilimwacha Mungu na kumfuata ibilisi. Sikutambua kuwa mtu huwa
ama yuko anamtumikia Mungu au anamtumikia shetani – hakuna
namna ya kusema ‘mimi siko kwa Mungu wala kwa shetani.’ Ukiwa
kwa Mungu unakuwa hauko kwa shetani. Ukiwa nje ya Mungu, moja
kwa moja unakuwa uko kwa shetani. Hakuna sehemu ya kati!
Hivi sasa ninatambua kwamba Mungu alikuwa muda wote
ananiangalia licha ya maamuzi yangu yote mabaya.
Katikati ya majira ya joto, nilipata kanisa na kuwa na marafiki
kadhaa. Hatimaye sasa nilikuwa na mtu wa kuzungumza naye
na angalau kutoka naye. New York ni sehemu ngumu sana kwa
Wakristo. Pia, hivi sasa ninatambua kuwa kumbe hata marafiki
zangu pale kanisani nao walikuwa wanapitia magumu mengi vilevile
kama mimi! Hata hivyo, kuwa wewe na kuombeana na kumtazama
Yesu yalikuwa ni mambo ambayo tulikuwa hatufanyi. Kutafuta
mafanikio ya kazi lilikuwa ndilo jambo tulilolipa umuhimu zaidi.
Jumapili moja nilikutana na mwanamume mmoja kanisani. Mara
moja nilivutiwa naye. Ninapotafakari sasa ... natambua kuwa mara
nilipoondoa macho yangu kwa Yesu, nilifanyika mtu rahisi sana
kushambuliwa na shetani. Hilo lilimpa nguvu juu yangu na kudhibiti
hisia zangu na mawazo yangu. Na kwa kuwa sikuwa na upendo kwa
Mungu moyoni mwangu, nilihitaji kitu mbadala. Nikawa nimevutika
kabisa kwa huyu mwanamume.
Pale nilipokuja kutambua kuwa uhusiano wangu naye hauwezi
kufika mbali, nilianza kumwomba Mungu na kusoma Biblia.
Hata hivyo, bado nikawa sikumwomba Mungu awe Bwana wa
maisha yangu tena. Nilitaka tu anisaidie kwenye matatizo yangu
niliyojisababishia mwenyewe. Kwa kule kutoyatoa maisha yangu
yote kwa Mungu, sikuwa na uwezo kabisa wa kuvunja ule uhusiano.
Sikujua wakati ule kwa nini sikuweza kumkatalia yule bwana
kunitumia mimi, na kumwambia ‘hapana’. Nilikuwa nimenaswa
kwenye hisia zangu mwenyewe na sikuwa na uwezo wa kutoka
humo. Nilijua kwa moyo wangu wote kuwa nilikuwa namtenda
Mungu dhambi.
Nilibakia nikiwa nimenaswa kwenye uhusiano huu kwa mwaka
mzima. Kwa kuwa huyu bwana hakuwa msomaji wa Biblia na
hakupenda kuzungumza kuhusu Mungu, mimi nami pia niliamua
kuacha kuyafanya hayo. Kwa hiyo, nikawa nimeenda mbali zaidi na
Mungu na hatimaye nikawa nimekuwa mwenyewe tu.
Baada ya mahafali yangu ya chuo, nilifanya kazi New York katika
kipindi cha majira ya joto. Nilipata kazi kwenye benki yenye
hadhi na nilikuwa na uwezo sana kwenye kazi yangu. Bosi wangu
aliniambia jinsi ambavyo alipenda kazi yangu na jinsi nilivyokuwa
bora na mwenye akili. Nilijawa na majivuno na kiburi hata zaidi.
Baada ya uhusiano wangu na yule bwana kuvunjika, nilijihisi kuwa
ninataka kugeukia kwenye kitu kingine ili kujaza uwazi uliotokea.
Bado nilikuwa najiona kuwa simhitaji Mungu. Nilikuwa bado nina
hasira naye kutokana na kutonipatia kile nilichohitaji. Ndipo kazi
yangu ikawa ndiyo mungu wangu. Nilimuabudu huyu mungu wangu
kwa bidii zote.
Kuishi Moscow…
Nilipoenda Moscow, nilipanga kufanya usaili na mabenki kumi
makubwa ya nje. Cha kushangaza, mambo yaligoma kabisa!
Sikuweza popote kupata kazi niliyoitaka! Najua sasa kuwa, sababu
mojawapo ya mimi kushindwa kwenye kila usaili ilikuwa ni tabia
yangu ya majivuno ambayo ilionekana kunisaidia sana wakati
nikiwa New York, lakini hakuna mtu aliyehitaji kiburi hiki kule
Moscow.
Niliishia kupata kazi ambayo niliichukia kabisa. Hata hivyo, ilibidi
niiache baada tu ya miezi mitatu. Niliweza kupata kazi nyingine
Moscow. Nilipoambiwa niache kazi yangu ya pili, kwa vile sikuwa
nafaa kabisa kwenye kazi hiyo, na pale nilipokataliwa kwenye
kila usaili niliofanya kule London, nilitambua kuwa Mungu alikuwa
anajaribu kila njia kunifanya nishtuke.
Nilipoteza kazi yangu Aprili (2004). Nilifanya usaili mara kadhaa,
lakini kazi sikupata. Kila jitihada ilikuwa haizai matunda kwangu!
Hatimaye Mungu alifanikiwa kuvuta umakini wangu. Nikaanza
kumwomba. Hata hivyo, nilijihisi kuwa hata nikitubu vipi, siwezi
kusamehewa. Nilipakua Biblia kutoka kwenye intaneti maana
nilishatupilia mbali Biblia zangu zote pale nilipoondoka New York.
Nikaanza kusoma Agano Jipya tena.
Siku moja, nilipojua kuwa usaili wangu wote umekwama, nilimlilia
Mungu ili anisaidie. Nilijiona sina tena matumaini kabisa.
Ndipo nilianza tena kusikia sauti ya ibilisi ikiniambia kuwa Mungu
hanipendi na hatanisamehe; na kwamba inabidi nijitupe kupitia
dirishani. Sauti ile ilikuwa ina ushawishi mkubwa na nguvu sana
kiasi kwamba nilidhani kuwa nitakuwa kichaa. Huku nikilia,
nilifungua Biblia na kuanza kusoma kwa sauti japokuwa nilikuwa
sielewi hata neno moja. Lakini sauti ile ikawa imetoweka!
Nilitambua kuwa nilikuwa nimemtenda dhambi Mungu sana na
nilihitaji kujua iwapo angenisamehe. Nikakumbuka hadithi za
kwenye Agano la Kale kuhusu Israeli – wafalme waliomtenda
dhambi Mungu, lakini wakatubu. Nikaanza kusoma hadithi zile.
Nikatambua kuwa majivuno yangu na kutotii zilikuwa ndizo dhambi
zangu kubwa mbili.
Katika kipindi cha kurudi kwangu kwa Mungu nilikutana na tovuti
yenye Shuhuda za Thamani. (www.precious-testimonies.com).
Nilisoma shuhuda karibu zote humo! Niliguswa sana na upendo
wa Mungu kwenye maisha ya watu mbalimbali. Niliguswa sana
na mateso na maumivu ambayo kila mmoja aliyapitia hadi kuja
kumpata Yesu Kristo. Lengo langu, nilikuwa nataka sana kujua
kama Mungu angeweza kunisamehe dhambi zangu.
Kupitia kwenye Biblia, na shuhuda zile, nilitambua kuwa sikuwa
nimempa Yesu maisha yangu yote na kwamba nilikuwa bado
nimeshikilia mambo yale niliyoyapenda na nilikuwa naogopa
kuyaachia na kumpatia Yesu. Pia nilitambua jinsi ambavyo
dhambi zangu zilimpatia shetani nguvu kubwa ya kuharibu maisha
yangu. Nilijifunza jinsi ilivyo kutembea kwenye njia ya ibilisi.
Sitakiubinafsi tena! Nilitaka kumtumikia Yesu japokuwa isingekuwa
rahisi na wakati mwingine ingekuwa vigumu sana. Lakini Yesu
hutoa uzima wa kweli na anajua kile kinachofaa kwa ajili yetu.
Mungu alikuwa na rehema na neema sana kwangu na Roho
Mtakatifu wake aliniongoza kwenye toba. Alihukumu majivuno
yangu na kukosa kwangu utii na uzinzi wangu. Tarehe 12 Juni,
2004, nilimpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha
yanguyote – si kwa sehemu yake tu! Nilimwambia achukue ndoto
na mapenzi yangu yote ya ubinafsi na aweke ndani yangu ndoto
na mapenzi yake. Nilimkabidhi hofu zangu zote. Nilimwambia
kuwa sikutaka tena kumtumikia shetani bali nataka kumtumikia
Yeye – Yesu. Maamuzi yangu yote ya nyuma yalinipeleka kwenye
kushindwa kabisa. Nilitaka sasa Yesu atawale maisha yangu na
kuyabadili apendavyo, na si vile ninavyotaka mimi.
Baada ya kufanya hivyo, nilijisikia faraja kubwa sana! Kwa mara ya
kwanza katika miaka mitatu, nilikuwa natembea barabarani huku
nikitabasamu na kupumua kwa uhuru tena. Nilijisikia mwepesi na
huru kabisa.
Nilikuwa nimeishi Moscow kwa karibu mwaka mzima, lakini nilikuwa
sina rafiki Mkristo hata mmoja. Kabla ya toba yangu, nilihudhuria
kanisa jingine lakini bado nilikuwa simfahamu hata mtu mmoja.
Kutokana na tabia yangu ya New York ya kutojiweka wazi, nilikuta
ni vigumu sana kuweka wazi mambo yangu ya moyoni kwa watu
wengine. Hii ndiyo sababu hakuna aliyejua kile nilichokuwa napitia;
na pia ndiyo sababu sikuwa na mtu wa kumweleza kuhusu mapito
yangu.
Baada ya uamuzi wangu huo, nilidhani kuwa ningeweza kurudi
kwa Mungu kwa nguvu za maombi yangu, toba na kusoma
Biblia mwenyewe. Lakini siku chache baada ya kuamua kumrudia
Mungu, nilihisi kama kuzimu yote imesimama kinyume nami!
Nilianza kuona kiumbe mwenye manywele mengi. Taswira hii
ilikuwa mbele za macho yangu muda wote kwa wiki kadhaa.
Nilikuwa ninaomba na kuomba na kusoma Biblia. Nilifunga
pia. Nilikiri damu ya Yesu juu yangu. Taswira hii mbaya wala
haikuondoka! Nilihisi kuwa ninachanganyikiwa. Usiku haikuwa rahisi
kulala. Sauti ilianza kuniambia tena kuwa Mungu hatanisamehe kwa
kuwa nimemkufuru Roho Mtakatifu na kutenda dhambi ambayo
Yesu hawezi kusamehe.
Siku moja niliamka nikiwa na uchungu na hasira. Nilihisi ule
mzigo na uzito tena. Nikaanza kumwomba Mungu anisamehe
na kumshukuru Yesu kwa kunifia. Lakini mashindano yangu
yakaendelea kuwa magumu zaidi na zaidi. Siku ile nilitambua kuwa
siwezi kushindana na ibilisi peke yangu. Nilihitaji msaada. Nilihitaji
sana mtu wa kuniombea.
Kweli imeshafunuliwa …
Pale nilipotambua kuwa nahitaji mtu wa kuniombea, niliamua
kupeleka mahitaji yangu ya maombi kwa watumishi wa tovuti
yaPrecious Testimonies. Watumishi hao si tu kwamba waliniombea,
bali pia walinipatia mwongozo muhimu sana kwa njia ya baruapepe.
Ilikuwa ni wao ndio walionifungua macho kuhusiana na ukweli
kwamba ibilisi yu hai na yuko duniani huku akifanya vita dhidi ya
Wakristo. Nilitambua kuwa yalikuwa ni mapepo ndiyo yaliyokuwa
yananiletea maumivu na mateso makubwa namna hiyo. Nimejifunza
pia kuwa ibilisi anawapepeta Wakristo wote kama ngano. Adui
aliwashambulia na kuwatesa Petro na Paulo na mitume wengine.
Anafanya hivyo hata leo kwa nguvu na ukali uleule!
Ulimwengu wa roho…
Nilipokuwa ninakandamizwa na adui mara baada ya kutubu
kwangu, Mungu alinifungua macho ili niweze kuona ulimwengu wa
roho. Kama nilivyosema, nilidhani kuwa ninachanganyikiwa pale
nilipoona kiumbe mwenye manywele mengi. Baada ya kutuma
mahitaji yangu ya maombi, nilijisikia amani kubwa. Nilijua kuwa
kuna mtu ameanza kuniombea.
Hata hivyo, niliendelea kuyaona mapepo yakinizunguka. Nilipoamka
siku iliyofuata, si tu kwamba niliweza kuyaona mapepo, bali pia
nilimwona malaika wangu. Taswira zilikuwa kama kioo. Nilikuwa
sina hofu hata kidogo. Niliweza kuona kwenye ulimwengu wa roho
kwa wiki kadhaa. Mungu alinifundisha masomo muhimu sana katika
kipindi hicho.
Somo la 1: Mapepo hayawezi kustahimili kusikia Neno la
Mungu.
Wakati fulani nilirudi nyumbani kutokea kanisani na nikawa nasoma
Maandiko. Niliinua macho na kuyaona mapepo kadhaa. Nikaanza
kumwomba Mungu anisaidie. Sikuwa nina hofu lakini nilikuwa tu
sijisikii amani kuyaona. Wakati nikiwa namwomba Mungu anisaidie,
nilisikia sauti moyoni mwangu ikisema, “Soma Maandiko.”
Nikauliza: “Nini?” Sauti ile ikarudia tena: “Soma Maandiko.” Nilitii
na nikaanza kusoma Maandiko. Lakini baada ya muda kidogo,
Mungu akaniambia: “Soma kwa sauti.” Nikawa kama
nimechanganyikiwa kidogo, lakini Mungu akarudia tena: “Soma
Maandiko kwa sauti.” Nilipoanza kusoma Maandiko kwa sauti
niliona kuwa mapepo yale yanafunika masikio yao kwa mikono yao
yenye makucha na kuanza kuhangaika kwa mateso makubwa. Hivi
ndivyo nilivyojifunza kuwa mapepo hayawezi kustahimili kusikia
Neno la Mungu. Neno la Mungu likitumika kwa imani na kweli, ni
silaha kubwa dhidi ya nguvu za giza.
Tangu hapo, nimejenga tabia ya kusoma Neno la Mungu kwa sauti.
Pia nimepakua kutoka kwenye intaneti Agano Jipya la sauti (lililo
katika fomati ya MP3). Nikiwa nyumbani, karibu muda wote huwa
nimefungulia Biblia hiyo. Huwa naisikiliza nikiwa nakula, napika,
najipamba, nk. Mara kadhaa Mungu amekuwa akielekeza umakini
wangu kwenye mistari ya muhimu sana na kunieleza maana yake
wakati nikiwa nakula au najiandaa kwenda kazini. Mwenzangu
mmoja aliniuliza ni rekodi ya aina gani hii ambayo huwa naisikiliza
karibu saa 24 kila siku. Nilimweleza na kumshirikisha sababu zangu
za kufanya hivyo, lakini najua kuwa hakunielewa kikamilifu.
Vilevile nilipakua Agano Jipya kwa ajili ya kompyuta yangu ya
mfukoni. Kila ninapopata nafasi, huwa najaribu kusikiliza Maandiko
niwapo kazini. Mara nyingi ninapopatwa na mashambulizi ya adui
nikiwa kazini, huwa naamua kusikiliza Biblia hiyo kama njia yangu
mojawapo ya kunisaidi kushinda vita.
Pia nilijifuza kwamba mapepo huteswa sana hasa na Kitabu cha
Ufunuo, na hususani sura ya 17, 18, 19, pale ambapo Maandiko
yanazungumzia kuhusu hatima yao ya mwisho. Hayawezi kabisa
kusikiliza mistari kuhusu Babeli ulioanguka na mistari kuhusu ibilisi
na manabii wake wa uongo kutupwa kwenye ziwa la moto.
Kuna mara kadhaa ambapo niliyatishia mapepo kuyasomea Kitabu
cha Ufunuo kama hayakuacha kunisumbua au kuondoka. Ni wazi
kuwa sikuyatishia tu, bali nilisoma sehemu hizo. Mbinu hii hata
hivyo si kwamba ndiyo jibu la kila kitu. Haikuhakikishii ushindi
kwenye kila shambulizi, lakini ni mbinu nzuri ya msaada upande
wetu. Mungu mara zote hunisaidia kupata mstari ambao unaweza
kunyamazisha kabisa sauti ya adui. Nimeshajifunza kuwa si kila
mstari utanyamazisha manyanyaso ya adui bali ni ile mistari
ambayo inahusiana moja kwa moja na tatizo lililopo. Ni kama ilivyo
kuinua upanga hewani na kupiga kushoto wakati adui yuko kulia.
Hiyo haisaidii kumshinda adui. Ni pale tu unapoelekeza mapigo
yako kwenye lengo ndipo utashinda mapambano. Hali ni ileile hata
kwenye mistari ya Biblia na uongo na unyanyasaji wa adui. Ndiyo
maana NI LAZIMA kujifunza Maandiko kwa bidii na kuweka mistari
kwenye kumbukumbu kichwani.
Katika majaribu ya Yesu ya siku 40 kule jangwani – pale shetani
alipomjaribu – je, Yesu alifanya nini? Alimjibu shetani kwa kutumia
mistari sahihi kutoka kwenye Neno la Mungu. Alishindana na
shetani kwa kutumia upanga wa Roho Mtakatifu, ambao ni Neno la
Mungu. Shetani anamnukulia Yesu Neno lakini si kikamilifu; anataja
nusu ukweli. Ukweli nusu mara zote huwa ni uongo uliokusudiwa
kudanganya wanadamu na kupoteza makusudi ya Mungu kwa ajili
ya wanadamu. Yesu alimnukulia shetani Kweli yote kwa 100% ...
na shetani hakuwa na kitu chochote cha kushindana na mbinu
ya mapambano ya Yesu. Shetani alishindwa kwa 100% kwenye
vita hivyo. Mungu hakuruhusu jambo hili liandikwe kwenye Biblia
kwa bahati tu ili kujaza nafasi. Shindana na mashambulizi ya
mapepo kwa kutumia kwa usahihi Neno la Mungu.
Lijue Neno ... Liamini Neno ... Fahamu lini pa kulitumia kwa
usahihi (usinukuu tu Neno nje ya uhalisia wa hali yako; mapepo
watakucheka!); kisha tamka Neno la Mungu kwa sauti, imba
nyimbo zinazotokana na Maandiko; omba Neno wakati wa maombi
yako na kuyaambia mapepo yanayokuzunguka, (japo huenda
hutakaa uyaone) – sikiliza Neno la Mungu linapoongelewa dhidi ya
matatizo yanayokukabili, lakini kwa mwongozo wa Roho Mtakatifu.
Mambo yote yanaweza kushindwa lakini haiwezekani kwa Neno la
Mungu kushindwa maana Roho Mtakatifu ndiye anayelifanya litende
kazi. Mungu hawezi kusema uongo; hivyo Neno la Mungu nalo
haliwezi kuongopa. Wanadamu hapa duniani wanaweza wasilielewe
Neno la Mungu, hivyo wakalitumia kimakosa katika hali zao, lakini
hilo haliwezi kutokea kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Hilo kila mara
hutokea kwa sababu ya nguvu za kipepo na mawazo ya kimwili ya
wanadamu ambao hawana ufunuo kamili wa Neno la Mungu, au
huenda wamelipindisha bila wao kujua, na kulifanya liseme kitu
ambacho Mungu hajasema. Kama Mungu alivyoandika: "Mbingu na
nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.” (Tazama:
Mt. 24:35; Mk 13:31; Lk 21:33). Mtu anapopokea ufunuo kamili
kwamba Yesu Kristo ndiye Neno, haishangazi basi kwamba
halitapita kamwe.
Somo la 2: Mapepo hujaribu muda wote kuingiza mawazo
maovu/ya udanganyifu kwenye akili yako.
Mara nyingi mapepo wanaficha sana udanganyifu wao kiasi kwamba
ni vigumu kutofautisha kati ya sauti na mawazo yao na yako. Hivyo,
kulisha ufahamu wako kwa Neno la Mungu kila wakati, kuomba na
kuwa mwangalifu ni mambo ya muhimu ili kuweza kutofautisha kati
ya mawazo yako na uongo wa adui.
Nilipojua ukweli juu ya hasira kali ya ibilisi na mapepo, nilianza
kutambua mengi ya mashambulizi yao yaliyofichika, hususani
mashambulizi ya kutaka kunishawishi nikubali uongo wao.
Nimegundua kuwa mambo mengi yanayokuja kwenye ufahamu
wangu hayatoki kwangu au kwa Roho Mtakatifu, bali ni kutoka kwa
mapepo.
Ukweli kwamba niliweza kuona jinsi ambavyo mapepo yanafanya
kazi kunizunguka mimi, kumenisaidia sana kutambua mashambulizi
yao na kupambana nao. Ni muhimu kabisa kutambua mashambulizi
yao mara tu yanapoanza na kutoyaruhusu kukamata akili yako.
Jambo la kwanza yanachofanya ni kupenyeza uongo kwenye akili
zetu. Kama uongo wowote ukikubaliwa na akili zetu, ni vigumu sana
kuja kuutambua baadaye na kupambana na mapepo. Si ajabu basi
Maandiko yanatuonya mara , yakitutaka kuwa macho kila wakati,
kuzifunga nia zetu, kukesha, kutofuatisha namna ya dunia hii bali
kufanywa upya nia zetu (kufanywa upya kwa Neno la Mungu).
Nimejifunza kuwa kudhibiti akili zangu ni jambo la lazima. Maana
silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata
kuangusha ngome; tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka,
kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira
ipate kumtii Kristo [Neno lake] (Tazama 2 Kor. 10:4-5). Ni
mashindano yasiyokoma kwangu kufanya kila wazo limtii Kristo
na kuharibu kila kitu ambacho mapepo yanajaribu kukiinua akilini
mwangu kinyume na elimu ya Kristo.
Ninakumbuka shambulizi moja ambapo akili yangu ilishambuliwa
kwa nguvu sana na adui na ilinibidi nisome Maandiko kwa sauti
mfululizo kwa saa kadhaa.
Mapepo yanaposhambulia akili, nimekuta pia kuwa kuna nguvu
sana ninapoyajulisha kuwa nimeshajua kwamba yananishambulia.
Kwa kuwa menyewe hupenda kutenda kazi zao kwa kificho
na hayapendi kuwekwa wazi, njia mojawapo yenye nguvu ya
kupambana nayo ni kuyafanya yajue kuwa umeyatambua.
Nakumbuka pia mapambano fulani ambapo nilijihisi kuwa
siwezi kabisa kuzuia manyanyaso ya adui. Mapepo yaliendelea
kunikumbusha jinsi ambavyo niliudhiwa na kuaibishwa kazini.
Yalikuwa yakiingiza akilini mwangu kila aina ya uongo yakitaka
kunifanya niwachukie wafanyakazi wenzangu na kumwasi
Mungu. Nilijaribu kila njia iliyokuwa ikiwashinda hapo kabla
kwenye mashambulizi mengine, lakini haikuwezekana. Yalikuwa
ni mashambulizi mfululizo ambayo sikuweza kupata namna ya
kushinda. Kisha asubuhi moja, mapepo yalipofanya mashambulizi
yao kama kawaida, Mungu alinifundisha mbinu yenye nguvu.
Niliyaambia mapepo kwamba, kila mara yatakaponikumbusha
jambo linalohusu kunyanyaswa kwangu na wafanyakazi wenzangu,
basi mimi nitawaombea, nitayafunga mapepo yanayowadhibiti
na nitamwomba Mungu awaimarishe malaika wa vita ambao
wanapigana kinyume na mapepo yale. Kweli kabisa baada ya
kuhakikisha kuwa nilikuwa sitanii juu ya kuwaombea wafanyakazi
wenzangu, mara moja mapepo yaliondoka na nikawa nimeshinda
vita ile. Ni wazi kuwa hata sasa bado naendelea kuwaombea
wafanyakazi wenzangu kila ninapokuwa kwenye maombi.
Somo la 3: Mapepo yanaathiri hisia zako ili kukudanganya.
(Angalizo muhimu: Kabla ya kuendelea na Somo la 3, napenda
nikutahadharishe kabla kuwa somo ambalo Mungu amenifundisha
juu ya hisia ni gumu kuelewa kinadharia bila mtu kupitia mwenyewe
kile nitakachosema. Napenda kusisitiza pia kwamba sisemi kuwa
mawazo yote mabaya yanatoka kwa mapepo. Pia, sisemi kuwa
ni lazima wakati wote tujisikie vizuri na tujisikie kuinuliwa. Sisi
binadamu ni viumbe wa hisia sana na tunaathiriwa na hali ngumu
na matokeo yake tunapata hisia za aina mbalimbali.
Hata hivyo, kuna nyakati ambapo hisia zetu hasi zinakuja
kutoka kwa mapepo moja kwa moja. Ni lazima wakati wote
tutafute mwongozo wa Mungu na kumwomba atufundishe jinsi
ya kutofautisha kati ya hisia zinazotoka kwetu na ambazo ni
mashambulizi ya mapepo na tumwombe atufundishe jinsi ya
kupambana na mapepo yanayotuletea hisia mbaya).
Nimejifunza kuwa mapepo yana uwezo wa kuathiri hisia zetu kwa
kutumia huzuni, kukata tamaa, kujiona hatuna maana, kuhisi kama
vile Mungu ametudanganya au ametuacha (na kwa upande wangu,
nilihisi kabisa kuwa Mungu amenisaliti) kuhisi kama vile Mungu si
wa kuaminiwa au Neno lake si la kuaminiwa, kuhisi Mungu hasikii
maombi yetu, achilia mbali kujibu; kuhisi kuwa Mungu hatupendi;
kwamba tumeshapoteza wokovu wetu, au kama tumemkasirikia
sana Mungu, kuhisi kuwa Mungu hatatusamehe, nk. Lengo la
mapepo ni kukuibia wewe na mimi furaha ya wokovu wetu ambayo
imo ndani ya mioyo yetu. Nimejifunza kupambana na uongo na
kusimama kwenye kweli ya Injili (furaha na amani nilizopewa
na Yesu katika roho yangu) badala ya kukubaliana na nguvu ya
udanganyifu ya mapepo inayotaka mimi niamini hisia zangu badala
ya kuamini Kweli na Neno la Mungu ... na kufanya Neno la Mungu
liwe ndiyo lenye mamlaka ya mwisho kwenye kila jambo.
Nakumbuka wakati fulani wa majira ya joto ambapo nilirudi
kazini nikiwa nimekata tamaa kabisa na nikayaona mapepo
yamenizunguka yakirukaruka kwa furaha kwa sababu hiyo. Jambo
hilo lilinighadhibisha mno Kama kuna kitu ambacho sikuwa tayari
nacho ni kuyapa mapepo nafasi ya kushinda na kufurahia kwenye
maisha yangu. Kwa hiyo, nilichofanya ni kuyatazama, nikavuta
pumzi kwa nguvu, nikala chakula cha jioni, kisha nikakusanya
nguvu zangu zote nilizokuwa nimezipoteza na nikasema kwa sauti:
“Mungu, asante kwa kazi na asante kwa furaha na amani niliyonayo
kwenye moyo wangu.” Nilienda chumbani kwangu na kuanza
kusoma Maandiko kwa sauti. Baada ya hapo sikuyaona tena yakiwa
yanarukaruka kwa furaha.
Nakumbuka pia wakati mwingine mapepo yalikuwa
yananishambulia kwa hisia za kukata tamaa pamoja na huzuni
kubwa. Nilishindana nayo sana. Huwa hayatumii sana mbinu hiyo
kwangu. Haina nguvu sana kwa sababu huwa najitahidi kutofuata
KAMWE hisia zangu. Huwa sisomi Biblia kwa vile tu eti NAJISIKIA
kufanya hivyo au kuomba kwa vile najisikia kufanya hivyo.
Ninasoma Neno na kuomba kwa sababu nimeamuriwa kufanya
hivyo na kwa sababu ninataka kuonyesha uaminifu wangu
kwa Mungu. Ninapotambua kuwa mapepo yananishambulia kwa
hisia hasi, mara moja ninamshukuru Mungu kwa ajili ya furaha na
amani niliyonayo katika roho yangu, nayakemea, kisha naendelea
na kile ambacho nilikuwa nimepanga kufanya.
Lengo kuu la mapepo katika kushambulia hisia zangu ni kutaka
kunidhibiti kupitia hisia. Sasa kama sitazifuata hisia zangu, lakini
nikafuata Neno la Mungu, mashambulizi yao yanakuwa ni kazi bure.
Ninajua kuwa mapepo huathiri si tu hisia zetu kwa kutujaza hisia
hasi, bali pia kwa kutumia hisia chanya za bandia ambazo ni
rahisi kwa mtu kuzitafsiri kuwa ni uwepo wa Mungu. Nimejifunza
kuwa Mungu hatendi kazi kupitia hisia zetu. Mungu hutenda kazi
kupitia Neno lake na imani yetu tu. Mapepo mara zote hutenda
kazi kupitia hisia za mtu kiasi kwamba mtu huyo atasoma Biblia
na kuomba pale anapojisikia kufanya hivyo na si kwa vile Mungu
ameamuru afanye hivyo. Ni vibaya sana kwamba Wakristo wengi
hawatambui kuwa kujisikia vizuri wakati wa kuomba au kuabudu,
haimaanishi kuwa hisia hizo ni lazima ziwe zinatoka kwa Mungu.
Ni nadra kwa Mungu kufanya jambo ili tu kutufanya tujisikie vizuri
kihisia. Yeye ana malengo mengine tofauti kabisa kwa ajili yetu.
Anataka kutufundisha kujilisha mioyo yetu kwa kutumia Kweli
(Neno la Mungu). Kweli mara zote hukubaliana na roho inayotafuta
kumpendeza Roho Mtakatifu. Kwa roho zetu na Roho Mtakatifu
kutenda kazi kwa pamoja na kwa kukubaliana kabisa, hisia
zetu zitaanza kufuata mstari, na ndipo itakuwa rahisi kutambua
ni nanianayeendesha hisia zetu.
Wakati fulani nilihudhuria ibada kwenye kanisa fulani. Nilihisi
hali fulani ambayo mwanzoni nilikuwa nikiita ni “uwepo wa Roho
Mtakatifu.” Baada ya ibada nilimwendea binti mmoja. Aliniambia
kuwa alifurahia sana “uwepo wa Bwana.” Mara moja nilijiuliza swali,
“Ni kweli ni uwepo wa Bwana? Je, Mungu wangu ninayemtumikia
anawaita watoto wake ili wawe wakimya tu? Au Mungu wangu
anawaagiza watoto wake wawe macho na wawe waombaji muda
wote?”
Hivi karibuni Mungu amenifundisha nisikubali kabisa hisia za “uwepo
bandia wa Bwana” unaokuja kutoka kwa mapepo. Kwenye sehemu
ya jumuiya ambako watu wanatafuta kuwa kwenye uwepo wa
Mungu, muziki wa sauti kubwa, kupaza sauti kwa watu pamoja
na spika kunaweza kusiwe chochote bali ni uchocheaji wa hisia
zetu hadi kiwango cha juu kiasi kwamba kunaweza kudhaniwa
kuwa ndio “uwepo wa Mungu” wakati siyo. Na inapotokea hivyo,
shetani anaweza kuleta udanganyifu kwa kila namna unaoweza
kuonekana kama ni utendaji kazi wa Roho Mtakatifu kumbe Roho
Mtakatifu anaweza kuwa yuko uani anatapika (yaani anaweza
kuwa anajisikia kinyaa kwa hali kama hiyo). Uwepo wa kweli wa
Mungu huwa unatambulika kwa mtu mmojammoja peke yake –
kwenye utulivu – katika ushirika binafsi na Mungu. Yesu hakuwa na
haja ya kuchochea watu kihisia kwenye sehemu ya watu wengi ili
kusikia kile ambacho Baba yake alitaka afanye. Mara zote ilikuwa ni
kwenye utulivu, mahali ambako hakuna vurugu. Hapo ndipo aliona
“uwepo wa Mungu.”
Lakini imekuwa ni kinyume chake ambapo kundi la Wakristo
“husubiri kwa kimya uwepo wa Roho” uwatembelee.
“Watetemekaji” na "wachekaji" na "waliaji" wamekuja na
kupita; na watakuja na kupita ... na kama udhihirisho wa nguvu
unaotokea wakati huo, hauzai matunda yaliyo wazi kwa dhambi
kuwekwa wazi na kutubiwa – roho haziokolewi – hakuna huduma
inayoburudisha ya Neno la Mungu – hakuna uponyaji wa hakika
ambao umethibitishwa na wataalamu wa afya – watu wanaanguka
kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni nguvu za Mungu, kitu ambacho
hakifanyi lolote zaidi tu ya kuvutia machoni mwa watazamaji.
Mapepo yanapewa uwanja wa kudhihirika kwa “wakristo” kwenye
ibada bila ya Wakristo hao kufuatiliwa kibinafsi. Wakristo ni lazima
wawe makini sana kukubali kwamba “miujiza hiyo inatoka kwa
Mungu.” Japokuwa Mungu amefanya na ataendelea kufanya yote
hayo niliyotaja hapo juu, shetani naye anaweza, na ataendelea
kuigiza mambo hayahaya.
Nimegundua kuwa mara mashambulizi ya adui yanapotambulika na
mtu akapambana nayo kwa bidii zote kwa kutumia upanga (Neno)
na ngao (Imani), adui huondoka mara moja. Ashukuriwe Mungu
atupaye kushinda kupitia Bwana wetu Yesu Kristo (1 Kor. 15:57) na
ambaye hutufanya kushinda (2 Kor. 2:14).
Kutambulishwa kwenye vitabu vya Rebecca Brown
Baada ya kutambua jinsi adui yangu alivyo na nguvu na ukatili,
niliamua kujifunza zaidi kuhusu vita vya kiroho kutoka kwenye
vitabu vya Kikristo mbali na kujifunza Biblia na kutoka kwenye
uzoefu wangu binafsi. Nilitambulishwa kwenye vitabu vya Rebecca
Brown na Mkristo mmoja kwenye kanisa nililoanza kuhudhuria mara
baada ya kuokoka. Nilitiwa moyo sana kuona kuwa kumbe mambo
mengi niliyojifunza katika vita vyangu vya kiroho yanathibitishwa
na Rebecca katika kitabu chake. Kupokea uthibitisho wa uzoefu
wangu limekuwa ni jambo muhimu sana kwangu kwa kuwa sikuwa
na mtu yeyote ambaye ningeweza kumshirikisha uzoefu wangu.
Zaidi ya hapo, ilikuwa ni muhimu pia kwangu kutambua kuwa
sikuwa peke yangu niliyeshambuliwa na adui. Wapo watoto wengi
wa Mungu wanaopitia mashindano makali kama yaleyale. Kujua hili
kumenisaidia kunyamazisha sauti ya adui aliyekuwa akininyanyasa
kutokana na ukweli kwamba “niko mpweke na peke yangu na sina
marafiki.” Kwa neema ya Mungu, hathubutu kufanya hivi tena,
maana ninajua kuwa siko mpweke (Yesu yuko nami daima) wala
siko peke yangu (watoto wengi wa Mungu nao pia wanashindana na
adui). Japokuwa sina marafiki wa Kikristo waliokomaa hapa Moscow
muda huu ninapoandika, najua kuwa hili limepangwa na Mungu
kama sehemu ya mafunzo yangu ili nijifunze kumtegemea Yeye
kunifundisha jinsi ya kufanya vita vya kiroho vyenye ushindi dhidi
ya nguvu za kipepo. Nisingependa watu wapate picha kwamba "ni
mimi naYesu tu"; kwamba siwahitaji Wakristo wengine kutoa
mchango kwenye maisha yangu, na kuniombea mimi pamoja na
mwito wa Mungu maishani mwangu - hapana. Isipokuwa kwamba
kwa sasa niko kwenye kipindi ambacho Mungu ananifundisha
mambo mengi moja kwa moja kutoka kwa Roho wake. Ni Mungu tu
ajuaye kile kitakachotokea kwenye maisha yangu yajayo.
Udanganyifu wa shetani makanisani
Baada ya kusoma vitabu vya Rebecca nilifanya utafiti kwenye
mtandao wa Google na kuiona tovuti yake. Kwenye tovuti
hiyo nilikutana na unabii/maono mawili kuhusiana na uchaguzi
mbalimbali wa Marekani yaliyoandikwa na mume wa Rebecca,
Daniel. Nilishtuka sana baada ya kufahamu kuhusu mbinu za adui.
Nimeshahuhudia uthibitisho mwingi kote kwenye habari za dunia
na kanisani kwamba unabii wa Daniel ulikuwa kweli kwa 100% na
unatoka kwa Mungu. Macho yangu yamefunguka na kuona kazi ya
adui iliyo ya kificho sana dhidi ya kanisa ikiwa ni pamoja na:
- Maombi yaliyojaa ubinafsi na kujitazama mwenyewe tu.
- Mahubiri yanayolenga upendo wa Mungu kama njia ya kunufaika sisi
na kile ambacho Mungu anaweza kututendea na si kile tunachoweza
kutenda katika kumtumikia na kuenenda kwa utii mbele zake.
- Unabii kuhusina na upendo wa Mungu usiokoma na si kuhusu haja
ya kuacha dhambi na kuwajali waliopotea.
- Mara chache sana nimesikia makanisani kwamba Wakristo
watateseka kwa ajili ya Yesu (na kiukweli, kadiri wanavyojitoa
kwa bidii kwa Mungu ndivyo huenda watateseka zaidi isivyo haki);
kwamba wanatakiwa kutambua na kujifunza kuukana ubinafsi wao;
kwamba mateso ni jambo linalotokea kila siku kwa namna moja au
nyingine na kwamba wanatakiwa kubeba misalaba yao ya mateso
yasiyo ya haki yatokanayo na kuonewa na kumfuata Kristo bila
kujali kuna maumivu kiasi gani – bila kujali gharama inayotakiwa.
- Kile ambacho nimeona kuwa kinasikika zaidi ni ujumbe wa
kificho wa kile ambacho Mungu atanitendea kama nikifuata kwa
usahihi “kanuni” fulani fulani na si kile ambacho ninatakiwa
kufanya kwa ajili yake ili kuenenda katika utakatifu na kuachana na
ubinafsi wangu ili kuwasaidia wengine kuja kwa Mungu na kukua
ndani ya Mungu.
Gharama ya kuwa Mwanafunzi wa Yesu
Septemba iliyopita, nilijitolea kufundisha masomo ya Biblia ili kutoa
picha ya gharama ya kuwa mwanafunzi wa Yesu pamoja na vita
vya shetani dhidi ya Wakristo. Nilichagua mistari inayojibu maswali
yafuatayo:
• Je, Yesu anaahidi utajiri kwa wanafunzi wake?
• Je, Yesu anaahidi afya kamili ya kimwili kwa wanafunzi wake?
• Je, ahadi ya kuteswa na kuteseka ilitimia kwenye maisha ya
Wakristo wa Agano Jipya?
• Je, Mungu anavumilia dhambi kwenye maisha ya Mkristo? Kwa nini
Wakristo waliteswa?
• Kwa nini Neno la Mungu linasema kuwa kila anayetaka kuishi
maisha ya uchaji Mungu atateswa?
• Je, Mungu anamruhusu shetani kuwashambulia Wakristo moja kwa
moja?
Niligundua kuwa wakati nikisoma Maandiko haya baadhi ya
watu walikosa utulivu. Nilipofika kwenye kusoma Maandiko
yanayoongelea kuhusu shetani kumpepeta Petro kama ngano,
kijana mmoja alipayuka kwa hasira. Alipinga kabisa mimi kusoma
mstari huo. Alisema kuwa mstari haukuwa unahusiana kwa namna
yoyote na Petro kumkana Yesu, na hakuniruhusu kuendelea kusoma
Maandiko zaidi ili kufafanua mstari huo. Nilikuwa sijawahi kukutana
na upinzani mkali namna hiyo kwa Neno la Mungu kutoka kwenye
kundi la waamini, na sikutaja chochote kinachonihusu mimi binafsi.
Nilikuwa nasoma tu kutoka kwenye Neno la Mungu!
Nilipomwomba kijana yule aniache angalau niendelee kusoma
Maandiko, alisema kuwa hataruhusu mafundisho yoyote ya uongo
kwenye kundi letu dogo. Wanakikundi wengine nao walinikabili na
kunitaka niwaeleze sababu hasa ya mimi kuwasomea mistari ile.
Karibu wakimbie kabisa kutoka kwenye nyumba yangu ungedhani
mimi ni mchawi. Niliumia na kulia.
Baada ya siku chache, Mungu alisema nami.
Aliniambia:“Watalikataa jina lako kama uovu. Thawabu yako ni
kubwa mbinguni. Niamini Mimi tu, Neno langu tu. Nitakuja na
kumlipa kila mmoja kwa kazi yake. Waombee. Vifungo nilazima
viharibiwe kwanza. Vifungo ni:
• Mwili
• Kupenda mali
• Kujipenda mwenyewe
• Starehe
Utateseka, usijipende mwenyewe, jikane mwenyewe, jifunze
kujikana katika kila kitu kinachopingana na Mimi. Soma Neno langu
na kuomba kila wakati. Nitajitukuza kupitia wewe. Hii itakuja kupitia
maumivu na mateso utakayopitia. Jifunze kuridhika na ulicho
nacho. Nataka kuwa chanzo pekee cha furaha yako na ridhiko.
Asiwepo mwingine. Omba kwa ajili ya kuenea kwa Neno langu
na kuharibiwa kwa kazi za adui. Jifunze kuniamini Mimi. Jifunze
kufurahi kwenye mateso yako. Omba kwa ajili ya kuharibiwa kwa
uongo na udanganyifu unaoharibu akili za wanangu. Nawapenda
wote sawasawa. Jiachie kwenye mapenzi yangu. Utukufu ni wa
kwangu peke yangu. Omba kila wakati, omba. Uharibifu unakuja
kwenye dunia hii. Wale wanaonitumikia ndio watakaopona; wale
wasionitumikia hawatapona. Omba.”
Baadaye nilipata uthibitisho ufuatao kwenye Neno la Mungu.
2 Timotheo 3:1-5:
Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho
kutakuwako nyakati za hatari.
Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye
kupenda fedha, wenye kujisifu,
wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao,
wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao,
wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali,
wasiopenda mema,
wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko
kumpenda Mungu;
wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao
nao ujiepushe nao.
Nguvu ya Mungu inatolewa si tu kuokoa, bali pia kuponya na
kukomboa na kuua asili yetu ya ubinafsi, anguko na kukosa
utii ...sio tiketi ya kusamehewa tena na tena huku mtu anaendelea
kutenda dhambi ileile tena na tena na kuyapuuza kana kwamba
toba ndogo tu inatakiwa kufanya kila kitu kiwe sawa kati yetu na
Mungu, halafu mtu anarudi tena kuyafanya matendo hayo hayo ya
uasi hadi atakapoenda tena kutubu. Unakuwa ni mduara unaojirudia
tena na tena kama kwamba Ukristo si zaidi ya kusema: "Unajua
nini? Naweza kutenda dhambi na ilimradi ninatubu, naweza kufanya
dhambi ileile tena na tena na kila kitu kinakuwa sawa tu kati yangu
na Mungu! Napenda kweli aina hii ya Ukristo!”
Hapana! Haitakiwi kuwa hivyo!
Tangu niokoke, nimekumbana na mashambulizi kadhaa kutoka kwa
adui ambayo yanakuja kupitia kwa mtu tunayekaa naye chumba
kimoja, wafanyakazi wenzangu, na hata washirika wa kundi langu
dogo la wapendwa, japo ndiyo yanakuja kutoka kwenye tamaa
za mwili wangu. Adui anatumia kila kitu na kila mtu kunijaribu
na kujaribu kuniharibu. Nimejifunza kuwa Yesu kweli alimaanisha
pale aliposema: “Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane
mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate.” (Luka 9:23).
Wakati mapambano yangu yanapokuwa makali kabisa, wakati
mwingine nahiksi kama vile msalaba wangu ni mzito kupita kiasi.
Ni vigumu sana kushinda mashambulizi ya mara kwa mara ya
adui, lakini Mungu amekuwa kila wakati mwaminifu na hunipatia
mstari unaofaa wa kumnyamazisha adui na amenipa hekima ya
kujishusha mbele zake na kutofunua kinywa changu mbele za wale
wanaonizushia mambo ya uongo.
Hivi karibuni nimegundua kwamba hata kwenye mapambano
makali, pale ambapo kila kitu na kila mtu anakuwa kinyume
nami INAWEZEKANA kubakia na furaha na amani ambayo Yesu
anatuahidi kwenye roho zetu, hata kama sijisikii furaha na amani
kihisia. Mapepo yanaweza tu kunidhuru kimwili na kihisia, lakini
kama nikisimama kwenye Neno la Mungu, hawawezi kunidhuru
moyo wangu ambako ndiko anakokaa Mungu. Neno la Mungu,
maombi na imani NI SILAHA ZENYE NGUVU SANA dhidi ya adui.
Kuingilia himaya ya shetani
Novemba 2004, nilikutana na jambo ambalo lilinipa msukumo wa
kujifunza zaidi kuhusiana na ibilisi na imani za siri. Nilisoma makala
kwenye gazeti kuhusiana na tovuti fulani ya Kirusi ambayo ilikuwa
inahamasisha watu kujiua. makala hayo yalikuwa yanahusiana na
vijana waliokuwa na majonzi na mawazo ya kujiua ambao hatimaye
walijiua kutokana na ushawishi wa tovuti hiyo. Makala yalisema
kuwa tovuti hiyo ilikuwa na taarifa nyingi za namna ambavyo
mtu anaweza kujiua kwa mafanikio. Vijana kadhaa waliosaidia
kuitengeneza tovuti hiyo, baadaye walikutwa wakiwa wamekufa.
Wazazi wao walimshitaki kiongozi/mwanzilishi wa tovuti hiyo.
Baada ya kusoma makala niliamua kuitazama tovuti hiyo. Nilikuwa
sijui kabisa kwamba tovuti hiyo ilikuwa ina uvuvio wa shetani na
kuendeshwa na waabudu shetani. Tovuti hiyo ni ya uovu kamili
ikiwa na picha za watu waliokufa na mandhari yenye giza ambayo
yanamfanya mtu asiyekuwa na huzuni au mfadhaiko aupate. Mbali
na mwonekano wa ajabu wa nje, tovuti hiyo unatoa giza la kiroho
ambalo linawaathiri moja kwa moja watu wanaoitembelea.
Nilisoma maelezo kuwahusu watu kadhaa humo ndani.
Wote walikuwa na historia zinazofanana. Walikuwa ni watu
walionyanyaswa sana wangali watoto; walitoka kwenye ndoa
zilizovunjika; walikataliwa na wazazi wao wakiwa wadogo;
hawajawahi kupata upendo au matunzo ya wazazi. Niliamua
kwenda kwenye sehemu ya kutoa maoni ili angalau niweze kusema
nao kwamba kuna mmoja anayeweza kuponya maumivu yao
na kuwaweka huru mbali na huzuni na fadhaa zao. kwa kutojua
kwangu, nilidhani kuwa huenda naweza kuwafikia watu wale.
Mtu mmoja akawa amevutiwa na kile nilichosema na akataka
kufahamu zaidi kuhusiana na kuwekwa huru. Hata hivyo, nilipoanza
kumweleza kuhusu kweli za Biblia, kila mara nilipoandika jina la
Yesu Kristo lilifutika. Kwa siku nzima nilizuiwa kabisa kuchangia
chochote kwenye ukurasa huo.
Usiku wa kwanza baada ya kuchangia kwenye tovuti ile, nilipatwa
na jinamizi baya sana! Mungu aliniamsha katikati ya usiku na
akaniambia niombe. Nilijawa na hofu kubwa kutokana na uwepo wa
uovu chumbani kwangu.
Siku iliyofuata nilijisikia kichefuchefu. Nilienda kwenye tovuti
ile asubuhi. Msichana mmoja aliandika swali, akiuliza ni dawa
gani atumie na ni kwa kiasi gani ili aweze kujiua. Nilijaribu
kumtumia ujumbe ili kumwambia amwite Yesu. Ujumbe wangu
ulizuiwa kwenda. Msichana yule alipata ujumbe kutoka kwa mtu
mwingine ukimshauri atembelee sehemu nyingine kwenye tovuti
ile inayoeleza kwa undani namna mbalimbali za kujiua. Nilitambua
kuwa, kwa makusudi, nilikuwa nimezuiwa kabisa kuandika ujumbe
wowote kwenye tovuti ile.
Niliamua kuwaeleza kundi lile letu dogo la maombi ili tuombe dhidi
ya ile tovuti na kwa ajili ya watu na kwa ajili yangu (maana nilianza
kupata majinamizi). Hata hivyo, hadithi yangu iliamsha chuki na
hasira nyingi! Wanakikundi walinizuia kwa ukali kuzungumzia
tena kuhusiana na tovuti ile na wakaanza kuhoji kama na mimi
nilikuwa na mawazo ya kutaka kujiua, na kama kweli nilikuwa
nimekombolewa kutoka kwenye mfadhaiko. Sikuamini kile
nilichokuwa nakisikia kutoka kwao!
Kisha kwa ukali waliniambia niondoke kwenye kikundi kile cha
Biblia kama nilikuwa sipendi vile walivyokuwa wakiomba sana kwa
ajili yao kibinafsi na kwa ajili ya wanakikundi wenyewe. Nilikuwa
sijawahi kutamka chochote juu ya kuondoka kwenye kikundi. Ni
wazi kwamba niliumia sana, nikalia na nikajaribiwa kuinuka na
kuondoka zangu. Hata hivyo, Mungu aliweka ndani yangu moyo wa
kubakia, kwa hiyo nilibakia pale.
Nilifurahi kwamba nilibakia kwa sababu mama mmoja mtu mzima
aliomba kwa ajili yangu. Aliniambia kuwa niliingia kwenye himaya
ya shetani bila ya kuambiwa na Mungu. Alinishauri kuwa niombe
tu kwa ajili ya watu wale wa kwenye tovuti, lakini akashauri kwa
nguvu sana kwamba niache kutembelea tovuti ile. Nilielewa kuwa
alikuwa sahihi. Nilijua kuwa siwezi kushindana na uovu niliokutana
nao. Haikuwa ni mashambulizi tu ya kawaida. Hapana. Ilikuwa
ni zaidi ya hapo – uovu mkubwa ambao usingekaa kimya kwa
sababu nimeingilia himaya yake. Nilizingatia ushauri wake. Hata
hivyo, majinamizi, hofu kubwa na uwepo wa uovu usiku viliendelea
kuniandama kwa muda.
Miezi miwili baadaye nilikuja kufahamu kuwa baadhi ya watu
wanaoendesha tovuti ile ni waabudu shetani. Kama ningejua hilo
kabla, nisingejaribu hata kuifungua tovuti ile. Namshukuru Mungu
kwa kuniweka salama wakati wa kukosa kwangu umakini. Mungu
aliniambia niendelee kuwaombea wale walio na mfadhaiko na kwa
ajili ya kuharibiwa kwa tovuti ile.
Baada ya tukio lile, niliamua kuijifunza mengi kadiri iwezekanavyo
kuhusiana na vita vya kiroho na adui na wale wanaojihusisha na
imani za siri. Najua kuwa kuingilia himaya ya adui bila mwongozo
wa moja kwa moja wa Mungu kunaweza kuwa ni jambo la hatari
sana. Katika kutafuta kwangu kufahamu juu ya ulimwengu wa
kipepo, nilinunua maandiko ya Howard Pittman, Jessie-Penny
Lewis na Rebecca Brown. Ninapendekeza kila Mkristo asome
kitabu kilichoandikwa na Jessie-Penn Lewis. Ni moja ya vitabu
vilivyoandikwa kwa uzuri na kwa undani kuhusiana na mambo
ya ulimwengu wa roho, kama ambavyo wengine wengi nao
wanakubaliana na hili. Nadhani Wakristo wote wanaweza kupokea
mafunuo mengi kupitia kitabu hiki, nacho kinaweza kupatikana kwa
kubofya: Hapa
Ufupisho wa masomo niliyojifunza kutoka kwa Mungu
Kwa kifupi, Mungu alinifundisha mambo yafuatayo:
1. Kila Mkristo amepangiwa mapepo na shetani yanayomfuatilia ili
yamharibu. Hakuna asiyekuwa nayo. Mungu kwa upande wake
ametupangia malaika mmoja au zaidi wa kutusaidia. Kama
tungeruhusiwa kuona ulimwengu wa roho unaotuzunguka, tutaona
malaika na mapepo wametuzunguka.
2. Mapepo hutufuata kila wakati. Wanafahamu udhaifu wetu, hivyo
wanapanga kutushambulia katika muda ulio mwafaka kwao. Ni
muhimu kwangu kufahamu udhaifu wangu na kumwomba Bwana
augeuze kuwa nguvu kwangu. Kujikana mwenyewe na kuachana
na kila kitu ninachokipenda sana ambacho hakimtukuzi Mungu
ni jambo la lazima. Ni njia pekee ya kupunguza uwezekano wa
kushambuliwa na adui.
3. Lengo la mapepo ni kunifanya nimuasi Mungu, kunifanya niwe mtu
wa kumnung’unikia, kumlalamikia, na kumkasirikia Bwana wangu
Yesu, na kuwadharau watu wa Mungu wasio na sifa mbalimbali.
Nilipogundua kuwa mateso na matatizo yangu yanatoka kwa adui
na si kwa Mungu, nilijifunza kuelekeza hasira zangu zote kwa
mapepo.
4. Mbinu ninayotumia kumaliza hasira zangu kwa mapepo pale
yanaponishambulia ni kwa kujitahidi kufanya kile ambacho Mungu
ananiagiza kufanya na kutompa kabisa adui nafasi. Ninajua kile
ambacho adui anataka kwangu na mimi siko tayari kumpatia kwa
hiyari yangu mwenyewe. Ni wazi kuwa haya ni mapambano makali
na magumu. Namjua yule ninayekabiliana naye; ni kiumbe mwenye
nguvu zaidi baada ya Mungu. Ni adui mwovu kabisa ambaye
mwanadamu anaweza kuwa naye hapa duniani. Sitarajii haki
yoyote kutoka kwa adui. Sitarajii kuwa ataniruhusu tu nisababishe
madhara kwenye ufalme wake kisha niendelee kuishi kwa furaha
tu hapa kwenye ufalme wake duniani. Nimeshahesabu gharama
zangu. Kila kitu maishani mwangu kiko hatarini. Najua kuwa adui
daima anadai, ama moja kwa moja au si moja kwa moja, ili Baba
amruhusu, yeye ibilisi anijaribu. Na pale ruhusa inapotolewa, najua
kuwa ibilisi atanivuta kuliko uwezo wangu. Lakini pia najua kuwa
Mungu ameahidi kuwa atanisaidia kushinda na kustahimili. Yesu
hakuwahi kuahidi kuwa ataniepusha na mateso, lakini aliahidi kuwa
atanifundisha kushinda na kustahimili. Niko tayari kubeba msalaba
wangu kila siku hadi mwisho, kushinda na kustahimili. Pia niko
tayari kupokea thawabu nzuri kwenye ufalme wa Mungu. Katika vita
vyangu siko tayari kurudi nyuma – sina mahali popote pa kurudia
nyumba – nina kusonga mbele tu!
5. Hakuna kitu kinachotetemesha ufalme wa shetani na jeshi lake la
mapepo kama pale watoto wa Mungu wanapoendelea kushikilia utii
wao kwa Bwana Yesu kupitia kumshukuru kila wanapoteswa na
kufedheheshwa na adui. Mungu amewapa mitume wake , maandiko
mengi "kuhesabu kuwa furaha" tunapoteswa isivyo haki na shetani
na kustahimili, maanathawabu yetu itakuwa kubwa mbinguni.
(Ibilisi muda wote anataka tuhisi kuwa Mungu ni katili kwa sababu
hatupatii thawabu zile tunazotaka kwenye maisha haya; na ni
lazima tuwe waangalifu ili tusiingiwe na hisia za kujionea huruma
kama kila kitu kinaonekana kiko kinyume nasi; vinginevyo ibilisi
anaweza kutumia hali hiyo kufanya shauku yetu ya kumtumikia
Mungu ishuke chini).
6. Kumbuka ... maisha haya ni mafupi mno kulinganisha na milele.
Mateso yoyote ambayo Mungu anaruhusu tuyapitie kwa miaka
michache hii tuliyo nayo hapa duniani, hata kama ni makali kiasi
gani, hayawezi kulinganishwa na uzito wa milele wa utukufu
yatakayotuletea. Hilo ni Neno la Mungu! (Tazama: 2 Kor. 4:17-18).
Kwa wale wanaojiona wamesalitiwa na Mungu
Kama kuna kipindi ulikuwa na moto na Mungu, ukiomba kwa bidii
na kusoma Biblia kwa bidii, lakini kidogo kidogo umeingiwa na
uchungu dhidi ya Mungu kwa sababu ya matatizo au mateso na
dhiki, mambo yafuatayo ni kwa ajili yako kibinafsi.
Kwa kuwa na mimi nimepita mahali uliko hivi sasa, na ninafahamu
uchungu wa kihisia na mfadhaiko unaokutesa, ningependa
kukupatia hatua kadhaa ambazo zilinisaidia mimi kupata uhuru
kutoka kwenye nguvu za shetani.
Njia yangu kuelekea kwenye kukombolewa:
1. Mungu alinisaidia kutambua kuwa Yesu hanichukii wala hanilaani.
Nilienda kutazama sinema ya “Mateso ya Kristo”. Kwa kutazama
mateso ya Kristo nilitambua kuwa Kristo hakunichukia hata kidogo.
Mapepo yalinishawishi kwamba Mungu alinichukia na kunilaani na
kwamba Yesu hakupata mateso makubwa ya kihisia. Uongo wao
uliota mizizi kwenye akili yangu. Niliteswa na uongo huu kwa miaka
miwili. Kupitia sinema ile, Mungu alivunja nguvu ya giza lile kwenye
akili yangu. Nilitambua kuwa Yesu, si tu kwamba hakunichukia, bali
pia aliteseka sana kwa ajili yangu. Hii ilikuwa ni hatua yangu ya
kwanza na ya muhimu sana kuelekea kwenye uhuru wangu.
2. Kwa kusoma shuhuda za waliookoka, nilielewa kuwa kumbe
sikuwa peke yangu kwenye mateso na dhiki. Kabla ya kuja kwa
Kristo, watu wengi walipitia mateso makali zaidi kuliko ya kwangu.
Mwanzoni mwa mchakato wa ukombozi wangu, mapepo yalishikilia
kwa nguvu sana akili yangu kiasi kwamba sikuelewa Biblia na
sikuweza kustahimili kusikiliza au kusoma Neno la Mungu. Hata
hivyo, nilikuwa na shauku ya kutaka kujua kama kulikuwa na
Wakristo wengine waliokuwa na mapito kama yangu. Wakati
nikitafiti kwenye mtandao wa Google, Mungu aliniongoza kwenye
tovuti ya Shuhuda za Thamani (www.precious-testimonies.com).
Wakati ninasoma shuhuda, Mungu alivunja uongo mwingine
uliokuwa umejikita kwenye akili yangu: nilitambua kuwa sikuwa
kamwe peke yangu kwenye mateso, kama ambavyo nilikuwa
nikiamini hapo kabla. Wapo wengi walioteswa zaidi yangu na
shetani. Kwenye shuhuda hizo, niliweza pia kuona namna shetani
alivyoharibu maisha ya wengine na jinsi Yesu Kristo alivyowaweka
huru na kuwapa maisha mapya.
Kweli kabisa “wao (Wakristo) walimshinda yeye (shetani) kwa
damu ya Mwana-Kondoo, na KWA NENO LA USHUHUDA WAO;
ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. (Ufunuo 12:11).
Baada ya kutubu, niliamua kuyatoa maisha yangu yote kwa Kristo.
Nilitia saini agano langu la kwanza na Mungu ambapo niliachana na
ndoto zangu zote za duniani; shauku zangu na matumaini yangu.
Nilimpa Mungu haki zangu zote ili aamue iwapo niwe na kazi au
la; kama nitaolewa au la. Katika agano langu nilijitoa kumtumikia
Mungu bila kujali niko mwenyewe au nimeolewa; niwe na kazi au
sina.
Wakati nikisoma Maandiko baada ya kuokoka kwangu, nimegundua
kuwa sababu kuu ya mimi kuharibu imani yangu ni kuwa sikuwa
nimefundishwa kwa usahihi mafundisho ya Yesu Kristo. Katika
karne ya kwanza, Wakristo waliteswa na kufa kwa ajili ya Kristo na
HAWAKUMKANA Kristo. Mimi sikuwa nimepokea shauku za tamaa
zangu za kimwili ndiyo maana nikamkana Kristo!!! Unadhani hilo
liliwafanya shetani na mapepo wafurahi?
Katika karne ya kwanza Wakristo walifundishwa mafundisho
ya Kristo kuhusu kuvumilia mateso kwa ajili ya Kristo. Nilikuwa
sikufundishwa au kusikia juu ya kuhesabu gharama ya kumfuata
Kristo. Sikuwa nimesikia juu ya kustahimili mateso kwa ajili ya
Kristo au kwamba inanibidi nijikane mwenyewe, nibebe msalaba
wangu na kumfuata Kristo. Sikuwa nimesikia au kufundishwa
kwamba inabidi nikane ubinafsi wangu ili kumfuata Yesu (achilia
mbali kujifunza namna ya kubaini ubinafsi hasa ni nini!)
Badala yake, katika vitabu vya Kikristo nilijifunza mafundisho ya
mashetani kuhusiana na Mungu kutaka kunipatia kila kitu ambacho
moyo wangu unakitamani. Kwa namna fulani labda sikuona sura
kwenye vitabu hivyo ambayo inanionya kuwa Mungu hatanipatia
kila shauku ya moyo wangu kama shauku hizo ni za ubinafsi na
si sehemu ya mpango wa Mungu kwa maisha yangu. Ilikuwa ni
makosa yangu mwenyewe kuamini mafundisho ya mashetani.
Sikufanya kile ambacho Mungu ameniamuru kwenye Neno lake.
Sikuijaribu kila roho kwa Neno la Mungu na sikuwa makini na
manabii wa uongo na walimu wa uongo. Matokeo yake, niliamini
mafundisho mengi ya mashetani.
Ilikuwa ni makosa yangu kuamini kila kitu nilichosoma kwenye
vitabu vya Kikristo. Na pale Yesu alipoacha kutimiza shauku za
moyo wangu za kidunia, na pale matizo yalipokuja maishani
mwangu kama Yesu alivyoahidi katika Yohana 16:13, sikujua
namna ya kustahimili. Kwa hiyo mwishowe nilianguka.
Hatima ya mafundisho ya mashetani ni kuwadanganya wateule na
kusababisha imani yao kuharibika.
Yafuatayo ni mafundisho ya mashetani ambayo niliyaamini.
Mafundisho haya ya mashetani yako kwenye makanisa mengi,
vitabu, kanda na CD na kwenye intaneti:
1. Kwamba Mungu anataka kukufanikisha kwa mali za kidunia na
kwamba ‘kuridhika na ulichonacho’ (Tazama: 1 Tim 6:8 na Ebr.
13:5) maana yake ni kuridhika na si chini ya dola milioni moja.”
2. Kwamba Mungu anataka kukupa kila haja ya moyo wako, na
mapenzi yake kamili ni kujibu kila ombi utakaloomba – huku akijibu
kama wewe unavyotarajia ajibu.” (Kwa maneno mengine, hakuna
haja ya kutilia maanani ubinafsi).
3. Kwamba shetani aliharibiwa kabisa msalabani, na kwamba shetani
hana nguvu juu ya maisha ya Wakristo. Hivyo, usipoteze muda
wako, hata wa dakika moja, kumfikiria. Vinginevyo, utakuwa
unampa utukufu ambao unamstahili Yesu.”
4. Shetani amefungwa na hawezi kuwagusa au kuwadhuru Wakristo
– kwamba anachoweza yeye ni kudanganya tu. Wakati wa Ayubu
ulishapita kwa sababu Yesu alishamshinda shetani msalabani.
Hivyo, shetani hawezi tena kuwashitaki Wakristo mbele za Mungu.
Kwamba shetani hawezi kuchukua chochote tena kutoka kwa
Wakristo.
5. Hauna haja ya kuteseka kwa ajili ya Kristo. Mateso si sehemu ya
Wakristo tena.
6. Kila wakati Mungu anataka uwe mzima kimwili bila kutilia maanani
mambo mengine. Vipi kama Mungu anataka kumpeleka mtu
huyo mgonjwa nyumbani mbinguni? Vipi kama Mungu anataka
kumfundisha jambo ambalo kwa njia nyingine hawezi kujifunza;
kwa mfano kujifunza kumtukuza Mungu katika madhaifu yake?
Vipi kuhusu watu wanaoshiriki meza ya Bwana bila kujihukumu na
kujikagua wenyewe sawasawa? Maandiko yanasema kuwa watu
wanaweza kuugua na kufa wangali na umri mdogo kutokana na
kutojihukumu wenyewe sawasawa. (Tazama: 1 Wakorintho 11:29-
31). Inaonekana kwangu kwamba hekima inatutaka tuangalie
uponyaji wa kimwili kama tunavyoangalia dhambi. Tunajua kuwa
Mungu anataka dhambi yote iondolewe kwenye dunia, lakini hilo
halitatokea hadi baadaye huko mbeleni. Japokuwa tuko salama
kuamini kwamba uponyaji wa kila aina hakika umo ndani ya
upatanisho kwa ajili ya watu wa Mungu, ni lazima tuwe na hekima
ya kutomwacha shetani aharibu imani yetu pale tunapomtafuta
Mungu kwa ajili ya uponyaji ... hasa pale uponyaji huo unapogoma
kutokea licha ya kuomba kwetu kwa bidii.
7. Kamwe usiseme, "Hata hivyo, si mapenzi yangu bali mapenzi ya
Mungu yafanyike maishani mwangu," kama hukupata kutoka kwa
Mungu kitu ambacho ulikiomba kwa Mungu. "Haujui mapenzi ya
Mungu kwa maisha yako, hivyo unatakiwa kuendelea kuomba zaidi
na zaidi ili Mungu akutendee kile unachokitaka.”
Yapo na mengine mengi zaidi – mafundisho ya kificho ya
mashetani yanayoendelea kufundishwa. KAMWE usiamini kila kitu
unachofundishwa kanisani au unachosoma kwenye vitabu vya
Kikristo kabla ya kukijaribu kama kinaendana na ushauri wa
Neno la Mungu katika Agano Jipya lote (pamoja na kanuni,
miongozo na amri za Agano la Kale ambazo hazipingani
na kweli iliyofunuliwa katika Agano Jipya, bali zinaiunga
mkono). Unafanyaje hivyo? Ibilisi anapenda kuchukua neno moja
au mawili kutoka kwenye Maandiko ambayo yanazua maswali
katika utekelezaji wake na kuyafanya yaseme kitu ambacho
Mungu hata hakukikusudia. Kila inapowezekana, acha Maandiko
yatafsiri Maandiko mengine. Acha hali ya kujirudia kwa mawazo
yaliyo kwenye Maandiko kujithibitishe kwenyewe ili kuumba imani
thabiti. Kutafsiri neno moja au mawili (au labda matatu au manne)
katika tafsiri zetu za Biblia za kileo kusichukuliwe kuwa ni lazima
kwamba kunaeleza kikamilifu maana iliyokusudiwa iliyokuwa
kwenye lugha za asili za Kiebrania na Kigiriki. Maneno, na namna
yanavyowasilishwa, yanaweza kubadilika kutoka utamaduni mmoja
hadi mwingine kadiri muda unavyopita. Roho Mtakatifu atathibitisha
kile kilicho cha muhimu kuamini na kipi sicho cha muhimu kutoka
kwenye Maandiko ili kumpendeza Mungu Baba kama tutanyenyekea
kiasi cha kutosha kukiri kuwa tunaweza kuwa tumekosea kutokana
na kile tunachoamini juu ya maeneo kadha wa kadha ya Biblia
ambayo hayaeleweki kirahisi.
Wakati huohuo, katika jitihada zetu za kuelewa na kutumia
sawasawa Neno la Mungu, tusisahau kamwe ukweli kwamba, ndicho
chanzo pekee cha kuaminika ambacho Mungu amewapa wanadamu
ili waweze kujua mapenzi ya Mungu. Neno la Mungu ndilo mapenzi
Mapenzi ya Mungu yamewekwa wazi kwenye Neno lake.
Hatuna cha kujitetea kwamba hatuwezi kujua mapenzi ya Mungu
yaliyowekwa wazi kwetu, (au miongozo ya namna ya kutafuta
mapenzi ya Mungu kwa ajili ya maisha yetu kibinafsi), kama hatujui
Neno la Mungu.
Huenda chapisho bora kabisa ambalo linaweza kumnufaisha sana
mtu katika kujifunza jinsi ya kujua kwa njia salama na ya hekima
kitu cha kuamini kuhusiana na Neno la Mungu linaweza kupatikana
kwa kubofya: Hapa.
Kumbuka, katika jamii tajiri, mafundisho ya mashetani ni nadra
sana kuwaambia watu kuwa ni lazima kuteseka kwa ajili ya
Kristo, ni lazima kumpinga shetani na ni lazima kujikana
mwenyewe, ubebe msalaba wako na kumfuata Kristo. Pale
ambapo kuna utajiri mwingi wa kimwili, mafundisho mengi ya
mashetani yana mvuto mkubwa kwa kimwili – karibu mara
zote huwa ni kwa ajili ya kile ambacho Mungu anaweza
kututendea na si kile ambacho tunatakiwa kutenda ili
kumpendeza Yeye.
Mafundisho ya mashetani karibu kila wakati huwa ni kwa ajili
ya kulisha tamaa zetu za kimwili, zenye ubinafsi; yanalenga
kupotosha maana na matumizi halisi ya Neno la Mungu; yanalenga
kushushia hadhi usahihi na uhalisi wa Neno la Mungu; yanalenga
kumpokonya Mungu utukufu anaostahili; yanalenga kuwadanganya
na kuwajaribu watu ili wamchukie Mungu wakati kumbe ni shetani
ndiye wanayetakiwa kumchukia.
Shetani anataka watu waamini kuwa jehanamu si halisi ili kusiwepo
na hofu yoyote ya Mungu na nia kuacha dhambi; kwamba mapepo
hawapo au kwamba hayana nguvu kabisa juu ya watu waliookoka
kwelikweli, maana kwa njia hiyo, Wakristo hawatamtafuta Mungu
kwa ajili ya kupewa uwezo wa kufanya kile wanachotakiwa kufanya
katika kusaidia kupambana na kazi za kipepo duniani na kwenye
maisha ya wapendwa wao. Orodha ya udanganyifu wa shetani
inaendelea na kuendelea ...
Shetani amejaribu, na hataacha kamwe kuendelea kujaribu,
kuwafanya watu wa Mungu wasitambue kuwa Neno la Mungu
lililoandikwa ndilo pekee lenye mamlaka ambalo Mungu analiafiki na
kulitia nguvu.
Hii ndiyo amri ya Mungu: Kwamba uyajaribu mafundisho yote
unayoyasikia kanisani au unayoyasoma vitabuni au kwenye
intaneti na kuwa makini na manabii wa uongo na walimu wa
uongo. Kama hujasoma sawasawa Agano Jipya bado, basi waendee
waelewa kadhaa tofauti wa Biblia wa kiprotestanti kabla ya
kuumba imani yako thabiti juu ya jambo lolote. Duka lolote la
vitabu vya Kikristo linaloheshimika linaweza kukutajia waelewa
hao. Kama hakuna duka karibu, bofya tovuti hii na kuwauliza.
Wanaaminika na wanaweza kukuelekeza kwenye mwelekeo
sahihi:www.gospelcom.net
1 John 4:1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho,
kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo
wengi wametokea duniani.
Philippians 3:2 Jihadharini na mbwa, jihadharini na watendao
mabaya, jihadharini na wajikatao.
Kumbuka: mafundisho ya mashetani yana uwezo mkubwa sana
ya kumharibu Mkristo kama ukiyaamini na kuyafuata. Mafundisho
ya mashetani yatakufanya usiwe na nguvu kwenye ufalme wa
Yesu na badala yake ukawa ni mtu wa kufuata tu ubinafsi wako au
yatafanya imani yako ife kabisa.
Shetani amejitoa kwa nguvu zote kufanya vita dhidi ya wafuasi wa
Kristo. Ni wale TU wanaofuata mafundisho sahihi ya Kristo ndio
wataweza kupona mashambulizi makali ya adui na kupokea “taji ya
uzima” kutoka kwa Mungu.
Ni lazima umwombe Mungu akufundishe jinsi ya kupambanua kati
ya uongo na kweli. Kumbuka kuwa kamwe hutaweza kushinda
uongo wa shetani kwa nguvu zako pekee. Ni kwa nguvu za Yesu TU
ndipo utaweza kuutambua uongo wa adui.
Nakutia moyo usome Biblia kwa bidii, kila siku. Mungu ndiye
Mwalimu BORA kabisa. Hakuna kitabu au mahubiri yoyote
yanayoweza kuchukua nafasi yote ya ushauri na mafundisho kutoka
kwa Mungu mwenyewe moja kwa moja. Shauku ya Mungu kwa
ajili ya watoto wake ni waijue kweli na kuweza kupambanua kati ya
jema na baya kama inavyosemwa kwenye Waebrania 5:14.
Mimi si pekee niliyeangukia kwenye uongo wa shetani; wako wengi
wanaopita kwenye matatizo kama niliyopitia mimi. Ni kwa sababu
tu ya rehema na neema kuu za Mungu ndiyo maana alinivuta nirudi
kwake na akanikomboa kutoka kwenye nguvu za shetani.
Ninamwomba Mungu atumie ushuhuda huu wangu kwa ajili ya
kueneza Ufalme wa Yesu na kuharibu ufalme wa shetani.
Endapo unanyanyaswa na nguvu za giza, au uko tayari kuachana na
Ukristo kwa vile unahisi kuwa Mungu amekusaliti, kama ambavyo
nami nilidanganywa na kuamini hivyo, unaweza kuniandikia
baruapepe. Nitafurahi kumtumikia Bwana wangu Yesu katika kujibu
maswali yako.
No comments:
Post a Comment